0 Chaguzi za Udiwani: CHADEMA yaitesa CCM



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeendelea kukiburuza Chama cha Mapinduzi (CCM) katika siasa, ambapo kwenye matokeo ya udiwani katika uchaguzi uliofanyika jana, chama hicho kimefanikiwa kutetea kata zake na kunyakua nyingine za CCM.

Hata hivyo uchaguzi huo ambao ulifanyika kwenye kata 29 katika halmashauri mbalimbali nchini, umemalizika huku vurugu kubwa zikitawala na kusababisha wafuasi wa vyama hivyo kuumizana.

Hadi tunakwenda mitamboni matokeo ya kata 14 yalionyesha kuwa CCM ilikuwa imefanikiwa kurejesha kata zake saba, huku CHADEMA ikinyakua kata sita, ambapo mbili zilikuwa za kwao na nne imewanyang’anya CCM na CUF ikiwa na kata moja.

Katika matukio ya vurugu, mbunge wa viti maalumu, mkoani Shinyanga, Rahel Mashishanga (CHADEMA), na katibu wa chama hicho jimbo la Nyang’hwale, mkoani Geita, Michael Ndege, wamenusurika kuuawa baada ya kuvamiwa na kisha kupigwa na kukatwa mapanga na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.

Viongozi hao walifanyiwa unyama huo kwa nyakati tofauti juzi na jana, ambapo Ndege alivamiwa juzi majira ya saa 3 usiku akiwa anaelekea kulala katika nyumba aliyofikia kata ya Lwenzela, saa chache baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni.

Inadaiwa kwamba akiwa njiani kwenda kulala alivamiwa na kundi la vijana waliokuwa wamevalia sare za CCM, kisha kumkata kwa mapanga na visu, jambo lililosababisha kutokwa damu nyingi na baadaye kukimbizwa hospitali ya wilaya ya Geita.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi juzi usiku kwa njia ya simu, Katibu wa CHADEMA wilaya ya Geita, Rogers Luhega, alisema kwamba kiongozi huyo alivamiwa na kundi hilo kwa mambo aliyodai ni ya kisiasa.

Kwa mujibu wa Rogers, baada ya tukio hilo waliomba msaada kwa askari polisi waliokuwa wakilinda usalama katani humo, lakini walikataa.

Hata hivyo, alisema usiku wa kuamkia Oktoba 27, mwaka huu, alikoswakoswa kuchomwa mshale na watu aliodai kuwa ni wafuasi wa CCM, ikiwa ni lengo la kudhoofisha nguvu ya chama chake katika uchaguzi huo mdogo kata ya Lwenzela.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Geita, Leonald Paul, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema kwa sasa wanafuatilia kwa undani tukio hilo na watu waliohusika ili sheria ifuate mkondo wake.

Kuhusu Mashishanga, inadaiwa kuwa jana majira ya asubuhi alivamiwa na kundi la vijana wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM wakati alipokuwa akitembelea kujionea upigaji kura linavyoendelea katika kata ya Mwawaza, jimbo la Shinyanga Mjini.

Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Vincent Nyerere, aliliambia gazeti hili kuwa mbali na Mashishanga kuvamiwa na kupigwa, gari lake pia lilipondwa kwa mawe na vioo kuharibiwa vibaya.

“Ni kweli nimeambiwa Mashishanga amevamiwa na kupigwa na wafuasi wa CCM wakati akitembelea kuona upigaji kura kata ya Mwawaza. Pia gari yake imepondwa na vioo vinaelezwa vimeharibika vyote,”alisema.

Nyerere aliongeza kuwa mbunge huyo alikuwa na mdogo wake ambaye alipigwa na kuteguka bega la kushoto na kuumizwa sehemu za mdomoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alipoulizwa kuhusuana na taarifa za kuvamiwa na kupigwa kwa mbunge huyo alisema hana taarifa juu ya tukio hilo na aliahidi kufuatilia zaidi.

Katika tukio jingine ambalo Tanzania Daima lilishuhudia, Katibu wa CCM wilaya ya Kahama, ambaye hakufahamika mara moja jina lake, aliingia kwenye kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Bugalama akiwa na sime mkononi.

Katibu huyo aliyekuwa akitumia gari namba T 507 BEW likiwa na nembo ya CCM, inadaiwa alifanya hivyo kwa lengo la kuwatisha mawakala wa CHADEMA waliokuwa wakisimamia kura za mgombea wao, lakini baadaye alitimuliwa.

Mkoani Ruvuma katika kata ya Mletele Manispaa ya Songea, nako wafuasi wa vyama hivyo walichapana kwa mapanga na fimbo na kusababisha zaidi ya watu watano kujeruhiwa wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo.

Tukio hilo ambalo lilitokea juzi saa tisa jioni huko katika kijiji cha Lihumbu, wafuasi wa CHADEMA akiwemo mbunge wao wa viti Maalumu, Chiku Abwao, walivamiwa na kupigwa na wafuasi wa CCM ambao wanadaiwa kuwa walikuwa na gari ndogo.

Hata hivyo wafuasi wa CHADEMA walifanikiwa kulikamata gari dogo la wafuasi wa CCM akiwemo Mwenyekiti wa UVCCM wa wilaya hiyo, ambayo ndani yake inadaiwa ilikuwa na mapanga, vipande vya nondo, mundu, fimbo na bundi akiwa hai.

Mmoja wa wafuasi wa CHADEMA Frank Mgao alisema kuwa baada ya kukamatwa gari hilo, askari ambao waliongozwa na Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, Nico Mwakasanga, waliwakamata na kuwapeleka kituo kikuu cha polisi cha Songea ambako wanaendelea kuhojiwa.

Mgao alisema kuwa baadhi ya wanachama wenzake na wanachama wa CCM wamejeruhiwa kwa kupigwa na panga sehemu mbalimbali za miili yao na wengine wamelazwa katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Ruvuma ambako wanaendelea kupata matibabu zaidi.

Matokeo

Wakati hali ikiwa hivyo, matokeo ya udiwani katika baadhi ya kata yalikuwa yakiendelea kutolewa huku CHADEMA ikiendelea kuiliza CCM kwa kuzitwaa baadhi ya zilizokuwa kata zake.

Jijini Arusha katika Kata ya Daraja Mbili, CCM ilipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyozoa kura 2192 dhidi ya 1315 za chama tawala.

CHADEMA wameweza kuzirejesha kata zao mbili za Nangerea jimboni Rombo, ambapo mgombea wao Frank Sarakana alijizolea kura 2370 dhidi ya 1134 za Dysmas Silayo wa CCM pamoja na ile ya Mtibwa, mkoani Morogoro.

Wilayani Sikonge katika kata ya Ipole, CCM walipoteza kata hiyo kwa CHADEMA iliyopata kura 577 dhidi ya 372 za washindani wao, na vilevile kuitwaa kata nyingine ya Lengali wilayani Ludewa iliyokuwa ya CCM.

CHADEMA pia ilikuwa ikiongoza katika kata ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, hadi tunakwenda mitamboni usiku.

Nayo CCM ilifurukuta kwa kuzirejesha kata zake za Msalato ya mkoani Dodoma, Bang’ata ya Arumeru Magharibi kwa kuwa 1177 dhidi ya 881 za CHADEMA, Mletele ya Songea CCM ilishinda kwa kura 950 na CHADEMA ilipata 295.

Pia CCM iliweza kutetea kata zake za Mwawaza mjini Shinyanga, Lwenzela mkoani Geita, Bungala wialayni Kahama na Bagamoyo mkoani Pwani kwa kuibwaga CHADEMA wakati Chama cha Wananchi (CUF) kilishinda kata ya Newala.

Nyimbo atimka CHADEMA

Aliyekuwa mgombea ubunge wa CHADEMA katika jimbo la Njombe Magharibi mwaka 2010, Thomas Nyimbo, jana alitangaza kukihama chama hicho.

Nyimbo ambaye amewahi kuwa mbunge wa CCM kwa miaka 10 katika jimbo hilo kabla ya kutimkia CHADEMA mwaka 2010, alisema hivi sasa atabaki kuwa mwanasiasa huru asiyefungamana na vyama.

Mbele ya mkewe, Mary Mwenga, alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona siasa za kushabikia vyama hazina tija kwa Watanzania walio wengi na badala yake zinawanufaisha viongozi wachache.

Nyimbo alifafanua zaidi akisema kuwa alichojiuzulu ni siasa za vyama, lakini si siasa moja kwa moja, huku akitamba kuwa yeye alizaliwa akiwa ni mwanasiasa, kiongozi na mtu ambaye mawazo yake yanahitajika.

Katika taarifa hiyo aliyoitoa kwa vyombo vya habari mithiri ya mhadhara, Nyimbo alitumia zaidi ya saa moja na nusu kuelezea mustakabali wa taifa na vijana kutokana na vyama vya siasa kuelekea kuwatumbukiza kwenye machafuko.

“Nimeachana na CHADEMA baada ya kubaini kuwa siasa za vyama hazina tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla na ni wakati huu sasa wa kuachana na dhana ya vyama vya siasa vituandalie sera na tunahitaji sasa itungwe sera ya kitaifa ambayo mgombea inabidi atueleze tukimchagua ataitekeleza vipi,” alisema Nyimbo.

Alisema kuwa ikiwa Katiba mpya inayoandaliwa hivi sasa itakuruhusu mgombea huru, atakuwa tayari kugombea ubunge tena kwenye jimbo lake la Njombe Magharibi, lakini kama Katiba hiyo itazuia fursa hiyo hatogombea tena wadhifa huo maisha yake yote.

Aliongeza kuwa baada ya kupatikana kwa Katiba mpya, inabidi itungwe sera ya taifa itakayolindwa kisheria, ambayo kila chama kitakachofanikiwa kuingia madarakani kilazimike kuifuata badala ya ilivyo sasa vyama vinaogelea hovyo.

Nyimbo alidai kuwa ameamua kujiondoa ndani ya chama hicho baada ya kubaini kuwa kinaenda kinyume na malengo yake kama kinavyojipambanua mbele za watu.

Alisema licha ya kuwaaminisha wananchi, hususan vijana kuwa ndio chama chenye kuleta mabadiliko ya kweli, viongozi wake wa daraja la juu akiwataja Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa wamekuwa wakijinufaisha binafsi.

Kuhusu CCM, Nyimbo alidai kuwa chama hicho kinajimaliza chenyewe kutokana na kuacha suala la rushwa kwenye chaguzi zake za ndani kuwa ndio kigezo muhimu cha kuwapata viongozi wake.


Source: Tanzania Daima

[Read More...]


0 Wabunge CUF wasusia Baraza la Wawakilishi



MAWAZIRI na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), jana walitoka ndani ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mjini hapa, wakati Mwakilishi wa Jimbo la Bububu, Hussein Ibrahim Makungu (CCM), alipokuwa akiapa.

Mawaziri na wabunge hao kupitia CUF, walitoka nje ya ukumbi huo jana asubuhi, baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, kutoa taarifa ya kuapishwa kwa mwakilishi mpya na kutaja jina la Hussein Ibrahim Makungu.

Baada ya Spika Kificho kutaja jina la Makungu, wawakilishi kupitia CUF, walitoka nje ya ukumbi kwa kile kilichoelezwa kuwa, hawakubaliani na ushindi wa Makungu, kwa kuwa uchaguzi uliomweka madarakani hivi karibuni, ulikuwa na utata.

Pamoja na CUF kususia tukio hilo, Makungu aliapishwa.

Makungu alipoapa, baadaye alizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi ulioko Chukwani, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Katika mazungumzo yake, Makungu alisema kwa sasa, ameapishwa rasmi na wananchi wa jimbo lake wakae tayari kwa maendeleo, kwani atatimiza ahadi zote alizoahidi wakati wa kampeni.

Akizungumzia kitendo cha wajumbe wa CUF kutoka nje wakati wa kuapishwa kwake, alisema hatishwi na tukio hilo, kwa kuwa anaamini alichaguliwa kihalali na wananchi wa Bububu.

“Kiukweli wenzetu wameonyesha hali ambayo si nzuri, lakini hata hivyo sisi CCM tumeliona hilo na tumejua wenzetu wapo katika mstakabali gani,” alisema Makungu kwa kifupi.

Akizungumza na MTANZANIA, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani katika baraza hilo, ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Chonga, Abdalla Juma, alisema yeye na wenzake, walilazimika kutoka nje ya ukumbi kwa kuwa hawamtambui Makungu kama mshindi wa Jimbo la Bububu.

“Sisi hatumtambui Hussein Ibrahim Makungu, kuwa ni Mwakilishi wa Jimbo la Bububu, mpaka hapo Mahakama itakapotoa maamuzi yake, kwa sababu tumefungua kesi mahakamani kupinga ushindi wake.

“Hatumtambui kwa sababu wengi wetu tuliushuhudia uchaguzi mdogo uliomweka madarakani, uchaguzi huo ulijaa udanganyifu wa waziwazi na kulikuwa na utumiaji mkubwa wa nguvu za vyombo vya ulinzi, vilivyokuwa vikiibeba CCM. Pia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, iliibeba wazi wazi CCM, kwa hiyo, hatuwezi kukubali ushindi wake, hadi hapo mahakama itakapoamua.

“Kwa maana hiyo, kama sisi tungeendelea kuwapo pale ukumbini, ingeonyesha kuwa tumeridhia kuwa Makungu ni Mwakilishi halali wa Bububu, kitu ambacho tunapingana nacho kwa asilimia zote

“Sasa basi, kitendo cha sisi kutoka ukumbini kwa upande mwingine, kitaionyesha Serikali Kuu, kwamba kuna mambo ambayo hayaendi vizuri kwa watendaji wake,” alisema Juma

Imeandikwa na Mtanzania Alhamisi, Octoba 11, 2012 (na Grace Shitundu), Zanzibar

[Read More...]


0 Siku mdau wako alipotembelea hifadhi ya Manyara kufanya utalii wa ndani



 

DSCN5278Mapokezi ambapo kuna ramani ya hifadhi yote. Hapa ni mtu yeyeote anaruhusiwa kutembelea bure na kujionea baadhi ya vivutio viachache vilivyohifadhiwa.

DSC00242Kwa mbali wanaonekana wanyama aina ya Kiboko wamepumzika

DSC00221Shughuli za utalii katika hifahdi hii hufanywa zaidi na magari ya aina hii ambayo ayanaelezwa kuwa na uwezo mzuri wa kuhimili mikikimikiki ya njia za vumbi

DSC00223Hiki ni kinyesi cha tembo, baadhi ya watu wanadai kinaweza kutumika kama dawa kwa namna mbalimbali

DSC00235Msafara wa tembo na vitoto vyao vikikatiza katikati ya tulipopaki magari. Kuna waliocheka kuna waliokaribia kulia na wengine kutaka kukimbia wakati tembo hao wakititisha mikonga yao jirani kabisa na kioo cha gari. Mhudumu alitufahamisha kuwa unapokuwa nadani ya hifadhi unapaswa kuwa na heshima na kuzingatia maelekezo yaote ya usalama. Kwa mfano, tembo kama hawa wakiwa wanazunguka gari yako, huna haja ya kuogopa…unatulia tu na kuacha wamalize shughuli yao. Tour Guider alituambia kuwa ni makosa makubwa sana kuwasha injini ya gari ikitokea hali ya namna hii au kujaribu kuondoa gari kwa nguvu.

DSC00265Mapumziko baada ya mizunguko ndani ya hifadhi

DSC00285Hapa ni mahali yanapatikana maji ya moto moja kwa moja toka ardhini. Maji Moto na Bonde la Ufa katika hifadhi ya Ziwa Manyara

DSC00300Mwenzetu katika msafara, Festo Tarimo akijaribu kuhakikisha kama maji hayo yanamoto kweli…

DSCN5284Kabla ya kuanza ziara ndani ya hifadhi ya Manyara

DSCN5305Kuna baadhi ya wanyama huwa ni adimu sana kuwaona maana mara nyingi huwahi kukimbia. Hapa tulibahatisha kuwaona wanyama aina ya Ngiri wamejichanganya na wanyama sampuli nyingine!

Posted by SeriaJr on Friday, October 12, 2012 0 Maoni yako?

Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook

Taswira Mtaani: Mafunzo ya Mgambo

DSCN5723Vijana wa Jijini Arusha walio katika mafunzo ya askari mgambo wakitembea “kikakamavu” kama walivyokuta na camera yetu muda mfupi uliopita katika barabara ya Old Moshi. Makampuni mengi ya ulinzi yamekuwa yakiwatumia vijana hawa baada ya kumaliza mafunzo kwa ajili ya shughuli za ulinzi katika majumba ya watu, maofisi, karakana au viwanda na hivyo kusaidia tatizo la ajira kwa kiasi fulani.

[Read More...]


0 FFU wa Ngoma Africa Band wamekinukisha ! AFRIKA-MESSE, Bremen Ujerumani




Ngoma Africa band Live Bremen,Afrika-MesseNgoma Africa band Live Bremen,Afrika-Messe
FFU waelekeza pa kushambuliaFFU waelekeza pa kushambulia
ffu wakiwa na mitutu yaoffu wakiwa na mitutu yao
ffu walipotua BremenFFU walipotua Bremen
kamanda Ras Makunja akiipanga safu ya FFUkamanda Ras Makunja akiipanga safu ya FFU
Wakina mama ndio waliokua mstari mbele ktk gwaride la FFUMashabiki wa Ngoma Afrika wakiserebuka mjini Bremen
********
KIKOSI kazi cha Ngoma Africa Band iliyozoeleka kwa tabia zake za kupagawisha washabiki wa muziki ughaibuni, Jumamosi ya 15.9.2012 Ngoma Afrika walifanya kweli katika maonyesho makubwa ya biashara ya Afrika-Messe, mjini Bremen,kule Ujerumani. Bendi hiyo maarufu ilipanda jukwaani na  kufanikiwa kuziteka nyoyo za washabiki kwa mara nyingine tena kwa kuwadatisha akili na muziki wenye raha kamili.
CD za bendi hiyo zimekamata nafasi ya juu katika vituo mbali mbali vya Redio ndani na nje ya Ughaibuni,baadhi ya vituo vya radio zikiwamo Redio maarufu nchi Ujeruamani Radio Funkhaus Europa na Radio  Mult-Kult ndizo zinarusha kwa fujo nyimbo za Ngoma Africa band, inayoongozwa na kamanda Ras Makunja wa FFU.Unaweza kuwasikiliza pia katika kambi yao at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com
Picha zote na Msemakweli wa NGOMA AFRIKA, Ujerumani
[Read More...]


 

Recent Comments

Popular Posts

Return to top of page Copyright © 2010 | Platinum Theme Converted into Blogger Template by HackTutors